New Tanzanian President Samia Suluhu Hassan addresses after swearing-in ceremony as the country's first female President after the sudden death of President John Magufuli at statehouse in Dar es Salaam, Tanzania on March 19, 2021. - Hassan, 61, a soft-spoken Muslim woman from the island of Zanzibar, will finish Magufuli's second five-year term, set to run until 2025, after the sudden death of John Magufuli from an illness shrouded in mystery. (Photo by STR / AFP) (Photo by STR/AFP via Getty Images)
in ,

Rais Samia kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa, Marekani

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Septemba 18, 2021 anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambapo tarehe 23 anatarajiwa kulihutubia baraza hilo.

Pamoja na Mkutano huo, Rais Samia pia atahudhuria  mikutano ya kilele ya kujadili masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) 

Aidha, anatarajiwa pia kukutana na wakuu wa nchi nyingine na viongozi wa mashirika ya kimataifa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania na nchi na taasisi zao.

IGP Sirro apangua Makamanda wa Polisi wa Mikoa

Balozi wa Zambia nchini Tanzania atumbuliwa