Makampuni ya kimataifa kuwekeza kwenye miundombinu nchini Tanzania

0
13

Kampuni ya huduma za majini AD Ports Group imesaini Mkataba wa Maelewano (MoU) na Adani Ports na SEZ Ltd, kampuni kubwa kwenye uwekezaji wa kimkakati wa miundombinu, huduma za baharini, huduma za kidigitali, eneo la viwanda na uanzishwaji wa vyuo vya baharini nchini Tanzania.

Kampuni hizo zimetia saini makubaliano hayo ili kukuza na kuboresha mfumo wa ikolojia wa usafiri wa baharini ambao utaifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara ukanda wa Afrika.

Mkurugenzi Mkuu wa AD Ports Group, Kapteni Mohamed Juma Al Shamisi amesema mkataba huo unaenda kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara barani Afrika.

Vitambulisho milioni 10 kuanza kutolewa Januari 2023

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Adani Ports na SEZ Ltd, Karani Adani amesema wanayofuraha kuungana na kampuni ya AD Ports Group huku akiamini wataenda kuleta mabadiliko katika sekta ya bandari na baharini.

“Tunafuraha kuungana na Kampuni ya AD Ports Group kwenye uandaaji wa miundombinu bora nchini Tanzania hasa katika sekta ya bandari na bahari, ambayo itaboresha na kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Tunaendelea kusaidia ajira za ndani pamoja na ukuaji wa uchumi wa Tanzania na nchi za Afrika Mashariki ambao utafanikiwa kwa uwekezaji wetu kupitia ushirikiano na AD Ports Group.” Karani Adani.

Send this to a friend