Serikali yaagiza atakayeuza sukari kwa zaidi ya TZS 3,200 kwa kilo ashtakiwe

0
26

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Ashatu Kijaji amewataka maafisa biashara wote nchini kukagua bei ya sukari duka kwa duka na atakayekutwa na bei zaidi ya shilingi 3,200 achukuliwe hatua za kisheria.

Waziri Kijaji ameyasema hayo alipotembelea kiwanda cha kuzalisha sukari cha TPC mkoani Kilimanjaro na kujionea shughuli za uzalishaji pamoja na kisikiliza changamoto walizonazo.

Amesema ni jukumu la maafisa biashara kutambua endapo mfanyabiashara yeyote atauza sukari juu ya bei kati ya shilingi 2800 na 3200 na kumchukulia hatua.

Dola & Mabadiliko ya Kodi vyapandisha Bei ya Mafuta

Amesisitiza kuwa ni jukumu la Serikali kulinda bidhaa yoyote inayotengenezwa nchini na kufanya juhudi za kila namna ili kuweza kuwasaidia wawekezaji na wafanyabiashara kuwa na mazingira bora na wezeshi ili kukuza biashara zao na kuwa na tija.

Aidha, amesema bidhaa zinazotengenezwa nchini zinatakiwa kuwanufaisha wawekezaji na wafanyabiashara wa ndani na biashara yoyotee inayofanyika nje ya nchi inatakiwa kuwa rasmi.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Utawala wa Kiwanda cha TPC, David Shiltu amesihi watanzania kuwa na Amani kwa kuwa sukari ipo sokoni ya kutosha na hakuna uhaba na uzalishaji unaendelea.

Send this to a friend