in ,

Nchi 10 Afrika zinazolipa wafanyakazi mishahara mikubwa zaidi

Ni tamanio la kila anayeajiriwa ama serikalini au kwenye sekta binafsi kupata kiasi cha malipo ambacho kitawezesha kumudu gharama za maisha. Hata hivyo, viwango vya mishahara hutofautiana kuliangana na elimu, uzoefu, eneo la kazi, cheo, na mambo mengine.

Kwa mujibu wa taasisi ya Statista, ambayo inajishughulisha na masuala ya masoko na walaji, hizi ni nchi 10 za Afrika ambazo zina kiwango kikubwa zaidi cha mishahara.

Licha ya serikali kuweka viwango hivyo, na kwa nyakati mbalimbali kuwachukulia hatua wanaovikiuka, bado wengine wamekuwa wakilipwa viwango tofauti kwa kuzingatia makubaliano ya mwajiri na mwajiri.

10. KENYA
Kenya imekuwa miongoni mwa Nchi iliyoingia kwenye orodha ya nchi zinazotoa mishahara ya juu kwa wafanyakazi Afrika, huku kiwango cha chini ni TZS 324,913.96 kwa mwezi.

9. ALGERIA
Kiwango cha chini cha mshahara Algeria ni TZS 350,442.91 kwa mwezi.

8. DR CONGO
Nchi hii imejiwekea kiwango cha chini cha TZS 357,405.36.

7. EQUATORIAL GUINEA
Kiwango cha chini  katika nchi hii ni TZS 464,162.80 kwa mwezi.

6. MAURITIUS
Mauritius imekuwa ikitoa kiwango cha chini cha TZS 556,995.36  kwa mwezi. Viwango hivyo vya mshahara huongezeka kila mwaka kulingana na kiwango cha mfumuko wa bei.

5. AFRIKA KUSINI
Nchi hii hutoa kiwango cha chini cha mshahara cha TZS 561,636.99 kwa mwezi.

4. GABON
Ni nchi inayopatikana katika eneo la Afrika ya Kati yenye wakazi 1,226,000 na wastani wa maisha ya miaka 50. Kiwango cha chini cha mshahara  ni TZS 594,128.38 kwa mwezi.

3. MOROCCO
Morocco inashika nafasi ya tatu kwa kuwa na kiwango cha chini TZS 652,148.73 kwa mwezi.

2.LIBYA
Nchi ya Libya imeingia kwenye orodha ya nchi zenye mishahara ya juu Afrika,  imejiwekea kiwango cha chini cha TZS 747,302.11 kwa wafanyakazi kwa mwezi.

1. SHELISHELI
Shelisheli ni kisiwa cha visiwa 115 katika Bahari ya Hindi, nje ya Afrika Mashariki. Kisiwa hiki kinashika nafasi ya kwanza katika mishahara ya wafanyakazi ambacho kiwango cha chini cha mwezi ni TZS 1,002,591.65

Uber yasitisha baadhi ya huduma zake Tanzania

Nigeria: Mama wa Osinachi Nwachukwu aeleza vitisho alivyopokea toka kwa mkwewe