in ,

Kamati ya Waamuzi: Kona waliyopata Simba dhidi ya Singida FG ni batili

Kamati ya waamuzi ya Zanzibar imesema kona iliyotolewa na mwamuzi wa mchezo kati ya Singida Fountain Gate na Simba SC katika nusu fainali ya pili ya Mapinduzi Cup haikuwa sahihi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Waziri Shekha, ameeleza hayo baada ya kikao kilichofanyika Januari 11, 2024, akisema kosa hilo ni la kibinadamu kwani waamuzi nao hufanya makosa.

Singida ilianza kupata bao la kwanza kupitia kwa Elvis Rupia na Simba ikasawazisha dakika za mwishoni, bao likifungwa na Fabrice Ngoma baada ya mwamuzi kutoa kona katika dakika za nyongeza.

Hata hivyo, matokeo ya mechi hiyo yaliamuliwa kwa mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare ya 1-1, na Simba SC kutinga hatua ya fainali ya Mapinduzi Cup kwa kuifunga Singida Fountain Gate kwa penalti 3-2.

Watanzania 22,000 walifariki kwa UKIMWI 2023

DCEA yapongezwa ukamataji wa dawa za kulevya