in ,

Kenya: Wake wenza wafikishana mahakamani kuhusu wapi mume wao atazikwa

Familia mbili nchini Kenya zimeingia katika mvutano mkubwa wa kisheria kuhusu mahali ambapo atazikwa aliyekuwa mume wa wanawake wawili ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 100.

Mzozo huo unaohusu kuzikwa kwa mzee huyo, Silas Igweta umefikishwa mahakamani baada ya mkewe wa kwanza, Grace Rigiri, kuchukuwa hatua ya kisheria kupinga uamuzi wa kumzika mwanaume huyo nyumbani kwa mke wa pili.

Grace Rigiri amefikisha suala hilo mahakamani akidai kuwa kulingana na ndoa yao, marehemu anastahili kuzikwa nyumbani kwake katika Kaunti ya Embu jambo ambalo limepingwa na familia ya pili, ikiongozwa na mke wa marehemu, Sarah Kathambi ikisisitiza kuwa marehemu aliachana na mke wa kwanza zaidi ya miaka 40 iliyopita na hivyo hakuna haja ya kumzika nyumbani kwake.

Mke wa kwanza ameeleza kuwa, kwa miaka 40 marehemu alionyesha wazi kwamba hakuwa na uhusiano wowote na mke wa kwanza na hakuwa na nia ya kurudi kwake na hata hivyo, marehemu alichagua kuzikwa katika eneo lingine ambalo ameainisha katika wosia wake.

Akamatwa kwa kuiba mtoto ili awaridhishe wakwe zake

“Baba yangu aliacha wosia ambao alikuwa ameandika kwamba angependa kuzikwa huko Lairang’i Mumui na kwa hivyo tukakubaliana kuwa wosia utasomwa siku inayofuata,” inasomeka katika kiapo cha mmoja wa watoto wa mke wa pili.

Familia ya pili inasisitiza kwamba talaka ilifanyika baada ya kifo cha marehemu, hivyo cheti cha ndoa kilichoshikiliwa na mke wa kwanza hakina maana kuhusiana na kuzikwa, pia imedai kwamba wametumia zaidi ya Ksh.5 milioni [TZS milioni 87] kumtibu mzee wao na familia ya kwanza haijachangia chochote wakati wa ugonjwa wake.

Mahakama imeamuru kusikiliza kesi hiyo siku ya Jumatano ikitazamiwa kutoa ufumbuzi katika mvutano huo.

Dkt. Mwinyi aondoa kodi ya sukari Zanzibar

Dkt. Mpango: Serikali inatarajia kupokea ndege mpya mbili