in , ,

Rais Samia: Tutawauzia majirani zetu gesi iliyoko nchini

Rais Samia Suluhu Hassan amesema gesi asilia ni bidhaa muhimu kwa nchi, hivyo ni lazima kuongeza uzalishaji na usambazaji wa gesi hiyo nchini kwakuwa mahitaji ya ndani bado ni makubwa.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mikataba ya mauziano na uendeshaji wa kitalu cha Mnazi Bay jijini Dodoma, amesema Tanzania imezungukwa na nchi ambazo bado hazijagundua gesi, hivyo imekuwa ikifanya mazungumzo na baadhi ya nchi hizo ikiwemo Uganda, Zambia na Kenya ili Tanzania iweze kuziuzia gesi.

Tanzania yasajili miradi ya uwekezaji trioni 4 kwa miezi mitatu

“Mahitaji ya gesi ni makubwa mno, makubwa ndani ya nchi na ukanda wetu wa Afrika Mashariki lakini na wenzetu kama Kenya pengine hata DRC wanaweza wakachukua kupitia lile bomba linalokwenda Uganda wanaweza wakarefusha likafika DRC wakatumia gesi ya Tanzania,” amesema.

Aidha, amesema kupitia sekta ya gesi, ni lazima wananchi wa Lindi na Mtwara waanze kuona manufaa ya miradi inayoendelea nchini ikiwa ni pamoja na kupewa vipaumbele wa ajira ambazo hazitahitaji utalaamu mkubwa.

Vile vile, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa kuwa na umiliki pamoja na maamuzi katika kutumia rasilimali zilizopo nchini.

Tanzania yasajili miradi ya uwekezaji trilioni 4 kwa miezi mitatu

Fanya mambo haya 8 kuepuka saratani ya shingo ya kizazi