in ,

Rais Samia: Wanawake wanaweza kufanya vizuri katika biashara na uwekezaji

Rais Samia Suluhu Hassan amesema anaamini kuwa katika upande wa biashara na uwekezaji, wanawake na wasichana wanauwezo mkubwa wa kufanya vyema katika eneo hilo endapo watapewa fursa na kuwezeshwa.

Hayo yameelezwa kwenye hotuba ya Rais Samia Suluhu iliyosomwa na Waziri wa Mambo ya Nje, January Makamba (Mb.) katika mkutano wa Mtandao wa Viongozi Wanawake Afrika (AWLN), Addis Ababa nchini Ethiopia ambapo amemwakilisha Rais Samia Suluhu.

Aidha, Rais Samia amepongeza AWLN kwa kuingia ubia na Umoja wa Afrika akiamini kuwa ubia huo utachangia katika kutengeneza wanawake wenye ujuzi na uwezo mkubwa katika uongozi ndani na nje ya Bara la Afrika.

Katika jitihada za kuwainua mabinti na wanawake kwenye nafasi mbalimbali za uongozi barani Afrika pamoja na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia, Tanzania inaungana na AWLN pamoja na Umoja wa Afrika (AU).

Tanzania imechukua hatua kwa kuwajumuisha wajasiriamali wanawake katika Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA), ambapo Rais Samia ameteuliwa kutoa hamasa na kuchangamkia fursa kwa makundi haya muhimu ya jamii.

Idadi ya wagonjwa wa figo Muhimbili yazidi kuongezeka

Rais Samia: Wanasiasa tufuate nyayo za Lowassa, tusitukanane