in ,

Ruto asema Gharama za ndege ya kifahari kwenda Marekani zililipwa na marafiki wa Kenya

Rais wa Kenya, William Ruto amesema ndege ya kifahari aina ya Boeing 737-700 ya shirika la Abu Dhabi aliyotumia kusafiri nayo kwenda nchini Marekani iliigharimu Kenya Ksh milioni 10 [TZS milioni 197.3] pekee na si Ksh milioni 200 [TZS bilioni 3.9] zinazoelezwa.

Ruto amesema baadhi ya marafiki wa Kenya ambao hakuwataja, walitoa ndege hiyo baada ya yeye kusema kuwa atasafiri na ndege ya shirika la Ndege la Kenya kutokana na bei ya chini ya ndege ya kukodi kuwa Ksh milioni 70 [TZS bilioni 1.3].

Rais Samia kufanya ziara ya kikazi nchini Korea

“Mimi ni kiongozi anayewajibika sana, hakuna jinsi naweza kutumia shilingi milioni 200,” amesema na kuongeza kuwa, “Baadhi ya marafiki zangu waliposikia kwamba nitasafiri na Shirika la Ndege la Kenya na tumejijengea sifa kubwa kama nchi, waliniuliza nitalipa kiasi gani, na baada ya kusema si zaidi ya Ksh milioni 20 walisema watachukua Ksh milioni 10.”

Rais Ruto amesisitiza kwamba Serikali yake inazingatia zaidi kubana matumizi akitaja kupunguzwa kwa asilimia 30 ya matumizi ya Ikulu, Ofisi ya Naibu Rais, na Waziri Mkuu wa Baraza la Mawaziri.

Ripoti yabaini dhahabu ya mabilioni ya dola husafirishwa kimagendo kutoka Afrika

Marekani yamwekea vikwazo Spika wa Bunge la Uganda na mumewe