in , , , ,

Nchi 10 za Afrika zinazokabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi, kiusalama na kisiasa kwa sasa.

Mwaka 2023 ulileta changamoto nyingi kwa nchi kadhaa za Kiafrika, ambazo zililazimika kuzoea mazingira magumu zaidi ya kiuchumi na kisiasa.

Kulingana na Ripoti ya mwaka 2023 ya Farihisi ya Mataifa Yaliyoyumba, iliyotolewa na Fund For Peace (FFP), baadhi ya nchi zilizopata alama kubwa zaidi kwenye ripoti hiyo, zinaonyesha hali ngumu ya kiutawala, uchumi, na usalama wa kijamii.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa, licha ya juhudi za baadhi ya nchi za Kiafrika kujenga uchumi imara na mifumo ya utawala thabiti, zipo changamoto kubwa ambazo hazijapatiwa suluhisho la kudumu.

Kupitia ripoti hiyo, inaonekana wazi kwamba jitihada za kimataifa na ndani ya nchi zinahitajika ili kushughulikia changamoto hizo zinazokabiliwa na nchi za Kiafrika.

Hapa chini ni nchi 10 zenye hali duni ya kiuchumi, kiutawala na kiusalama barani Afrika, kulingana na Fund for Peace.

  1. Somalia
  2. Sudan Kusini
  3. DR Congo
  4. Sudan
  5. Jamhuri ya Afrika ya Kati
  6. Chad
  7. Ethiopia
  8. Mali
  9. Guinea
  10. Nigeria

Rais Samia afanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali

Vilabu vitatu ikiwemo Azam vyapigwa faini kwa vitendo vinavyoashiria ushirikina