in ,

Ruto akataa kusaini Muswada wa Fedha 2024

Rais wa Kenya, William Ruto amesema hatatia saini Muswada wa Fedha wa 2024 baada ya Wakenya kuupinga vikali muswada huo na kufanya maandamano ya kuishinikiza Serikali, yaliyopelekea vifo kadhaa na uharibifu wa mali .

Mandamano hayo yameongozwa na vijana wa Kenya, ambao wanasema mapendekezo ya kodi yataongeza mzigo kwa wananchi ambao tayari wanakabiliwa na hali ngumu.

Akizungumza Ikulu leo, Rais Ruto amesema kuwa baada ya kuwasikiliza Wakenya ambao waliukataa kwa wingi Mswada huo, ameamua kutoidhinisha muswada huo kuwa sheria.

“Baada ya kutafakari kuhusu mazungumzo yanayoendelea kuhusu maudhui ya mswada wa fedha wa 2024, nitakataa kuidhinisha mswada huo. Kwa hivyo, sitatia saini Mswada wa Sheria ya Fedha wa 2024 na utaondolewa na nimekubaliana na wanachama hawa, huo utakuwa msimamo wetu,” amesema.

Aidha amesema atawapa nafasi vijana wa Kenya ili kusikia mitazamo yao na kukubaliana nao katika katika baadhi ya maeneo ya vipaumbele vyao.

Katika hotuba yake, Rais Ruto pia ametoa wito kwa Serikali ya nchi hiyo kuchukua hatua za haraka za kubana matumizi ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

“Ninaelekeza hatua za haraka zaidi za kubana matumizi ili kupunguza matumizi, nikianza na Ofisi Kuu ya Rais na kuendelea hadi kitengo kizima cha serikali,” amesema Rais Ruto.

PDPC: Wanaofunga CCTV kamera maeneo ya faragha wanakiuka sheria

Polisi kuwasaka waliomteka na kumjeruhi mfanyabiashara Sativa