in

Serikali: Maboresho yaliyofanywa na TANROADS kwenye mizani yamedhibiti mianya ya rushwa barabarani

Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imekamilisha ujenzi wa mzani mpya wa kisasa wa Mikumi uliopo barabara kuu ya Morogoro – Iringa, pamoja na maboresho katika mizani ya mikese uelekeo wa barabara ya Dar es Salaam – Morogoro kwa gharama ya shilingi bilioni 1.9, hatua ambayo imesaidia kumaliza msongamano wa magari katika barabara hizo.

Meneja wa TANROADS mkoani Morogor,o Mhandisi Alinanuswe Kyamba ameyasema hayo leo mara baada ya kutembelea na kukagua shughuli za ufanyaji kazi zinazofanywa katika Mzani wa Mikumi katika barabara ya Morogoro-Iringa, mzani wa Dakawa katika barabara ya Morogoro-Dodoma na mzani wa Mikese barabara ya Morogoro-Dar es Salaam.

Kyamba amesema maboresho hayo yameenda sambamba na kuweka vifaa maalum (Sensor) ambavyo vitafanya kazi ya kuchuja na kutoa taarifa ya uzito wa gari husika, ikiwa limezidisha mzigo, ambapo litalazimika kupita kwenye mizani na kama halikuzidisha basi linaendelea na safari moja kwa moja.

Amesema ili kukabiliana na vitendo vya rushwa serikali kupitia TANROADS imeamua kujikita kwenye utengenezaji wa teknolojia kwa kufunga mifumo ya CCTV kamera na mifumo ya usimamizi wa taarifa kwenye maeneo yenye mizani za kupima uzito wa magari barabarani jambo ambalo limepunguza kwa kiasi kikubwa “kama sio kumaliza kabisa kadhia ya rushwa barabarani.”

Ameongeza kuwa kupitia mifumo hiyo, TANROADS Makao Makuu na Wizara ya Ujenzi ina uwezo pia wa kuona kile kinachofanyika kwenye mzani na pale itakapobainika kuna uvunjivu wa sheria au viashiria vya rushwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi watu wanaohusika na vitendo vya rushwa.

Polisi kuwasaka waliotoa taarifa ya mgomo Kariakoo

Nafasi 102 za Ajira Serikalini