in , ,

Serikali: Rais Mwinyi ataongoza kwa kufuata katiba

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema Rais Dkt. Hussein Mwinyi ataendelea kuheshimu utaratibu uliowekwa wa Rais kuchaguliwa kila baada ya miaka mitano na kuwasihi watu wote wenye mawazo tofauti na hayo kufunga mjadala huo.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ni kufuatia maoni yaliyotolewa hivi karibuni kupendekeza Rais Mwinyi aongezewe muda wa kubakia madarakani kwa miaka saba badala ya mitano ambayo imeainishwa katika Katiba ya Zanzibar.

“Maoni hayo yamekwenda mbali zaidi hata kutaka Uchaguzi Mkuu wa mwakani kumchagua Rais wa Zanzibar usifanyike, jambo hili halina tija wala faida kwa nchi yetu na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye kufuata misingi ya demokrasia,” imeeleza.

Aidha, Serikali ya Zanzibar imesisitiza kuwa Rais Mwinyi ni muumini wa kufuata Katiba na Sheria za nchi, hivyo maoni hayo si ya Rais Mwinyi wala siyo ya Chama cha Mapinduzi Zanzibar.

Serikali yatangaza nafasi 231 za Ajira Shirika la Reli, NIT

Mashirika 10 ya ndege yanayofanya vizuri zaidi barani Afrika mwaka 2024