in ,

Tabora United hatarini kufungiwa uwanja wa nyumbani kwa kuvunja kanuni za ligi

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imesema imeazimia kuufungia uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kutumika kwa ajili ya michezo ya nyumbani ya klabu ya Tabora United endapo matukio ya vurugu na uvunjifu wa kanuni za ligi yataendelea kushamiri uwanjani hapo.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema matukio mengine ambayo yanaweza kusababisha adhabu hiyo ni pamoja na hila na vitendo visivyo vya kiuanamichezo vinavyofanywa na watoto waokota mipira (ball kids), walinzi wa uwanjani (stewards) na watoa huduma ya kwanza (first aiders).

Aidha, TPLB imeitoza klabu ya Tabora United faini ya shilingi milioni moja kwa kosa la mashabiki wake kuwafanyia vurugu viongozi wa klabu ya Biashara United kwa kuwapiga na kuwaumiza pamoja na kuvunja vioo vya basi dogo walilokuwa wanalitumia walipokuwa wakielekea kwenye kikao cha kitaalam cha maandalizi ya mchezo (MCM).

“Klabu ya Tabora United itawajibika kulipa gharama za matibabu ya viongozi walioumizwa pamoja na uharibifu wa basi dogo lililovunjwa vioo,” imesema.

Jeshi la Polisi lapiga marufuku kampuni za ulinzi kutumia Gobore

Waziri Makamba ashiriki mkutano wa 45 wa Baraza la Mawaziri wa EAC