in

Aliyejirekodi akimkashifu na kuchoma picha ya Rais Samia akamatwa

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia Shadrack Yusuph Chaula (24), mkazi wa Kijiji cha Ntokela, Kata ya Ndato Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa kosa la kumkashifu Rais Samia Suluhu na kuchoma moto picha yake.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Benjamin Kuzaga amesema baada ya video hiyo kusambaa katika mitandao ya kijamii, Jeshi la Polisi lilifanya ufuatiliaji na hatimaye kumkamata kijana huyo ambaye anajishughulisha na sanaa ya uchoraji.

“Mtuhumiwa huyo amekatwa na yuko kituo cha Polisi cha Tukuyu Wilaya ya Rungwe huku taratibu za kiupelelezi zikiwa zinakamilishwa na kisha jalada kupelekwa kwenye ofisi ya mkuu wa mashtaka katika wilaya hiyo na baada ya hapo atafikishwa mahakamani,” amesema Kamanda.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera kuliagiza Jeshi la Polisi kumkamata kijana huyo ndani ya saa 24 na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Daraja la Magufuli kukamilika Desemba mwaka huu

TANESCO: Ongezeko la kodi ya majengo kwenye LUKU ni madeni ya nyuma