in

Daraja la Magufuli kukamilika Desemba mwaka huu

Daraja la J.P. Magufuli (Kigongo – Busisi) lenye urefu wa Kilomita 3.0 na barabara unganishi Kilomita 1.66 linatarajiwa kuanza kutumika Desemba 30, 2024 likiunganisha Barabara Kuu ya Usagara – Sengerema – Geita zenye urefu wa Kilomita 90.

Daraja hilo linajengwa urefu wa kilometa 3.0 upana meta 28.45; unaojumuisha njia mbili za magari zenye upana wa meta 7.0 kila upande, njia ya maegesho ya dharura meta 2.5 kila upande, njia za watembea kwa miguu meta 2.5 kila upande, eneo la kati linalotenganisha uelekeo tofauti wa barabara meta 2.45, kingo za magari meta 0.5 kila upande, na kingo za watembea kwa miguu meta 0.5 kila upande.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa ujenzi wa Daraja hilo, Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Paschal Ambrose amesema mradi huo umetoa jumla ya ajira 29,211 tangu kuanza kwake Februari 25, 2020 ambapo asilimia 93.33 sawa na ajira 27,262 ni wazawa, na ajira 1949 sawa na asilimia 6.67 ni wageni.

Amebainisha kuwa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 88.61 dhidi ya asilimia 91.70 ya Mpango kazi Na. 5 ulioidhinishwa huku vifaa na mitambo ya ujenzi vilivyofika eneo la kazi hadi sasa vimefikia asilimia 99.

Aidha, ametaja faida zitakazopatikana baada ya kukamilika kwa daraja hilo kuwa ni pamoja na kupunguza muda wa kusafiri na uwepo wa uhakika wa usafiri masaa 24, kuondoa msongamano wa magari uliokuwa unatokea kwenye feri, pia litakuwa kivutio muhimu kwa Mkoa wa Mwanza na nembo kwa nchi ya Tanzania.

Rais Samia kugharamia matibabu ya Sativa

Aliyejirekodi akimkashifu na kuchoma picha ya Rais Samia akamatwa