in , ,

Rais Samia: Serikali na taasisi za kidini zishirikiane

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan anasisitiza ufanyaji kazi kwa ushirikiano kati ya Serikali na Taasisi za Dini nchini ili kuendelea kujenga amani, umoja na mshikamano.

Amesema hayo leo wakati akiwasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Rais Samia kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Wolfgang Pisa ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, kwenye makazi ya Askofu, Mtanda mkoani Lindi, ambapo ameeleza kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na taasisi hizo ambao huleta matokeo chanya kwa ustawi wa Taifa.

“Tunashukuru tunapata ushauri, yapo mambo ambayo mnayafanya na kuiwezesha nchi hii iendelee, mshikamano wetu ndani ya nchi, umoja wetu ndio unaozaa utulivu na amani tuliyonayo.

Wakati wote utakapokuwa na jambo ambalo unadhani Serikali inahitaji kushauriwa uwe huru na wakati wote unapoona kwamba unahitaji kuunganisha nguvu na Serikali, sisi tutakupa ushirikiano,” amesema.

Kwa upande wake Askofu Pisa amemshukuru Rais Samia kwa salamu za pongezi za kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa TEC.

Bei ya mafuta ya petroli yashuka; hizi ni bei mpya kwa mikoa yote

Rais Samia: Tumedhamiria kutatua changamoto za wafanyabiashara