Wanafunzi darasa la 3 watumia uzazi wa mpango

0
58

Utafiti uliofanywa katika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi kati ya mwaka 2019 hadi 2021 umebainisha kuwa, baadhi ya wanafunzi katika shule za sekondari Mkoani humo waliopo kidato cha kwanza na pili wamegundulika kutumia vipandikizi na vidonge vya kuzuia mimba tangu wakiwa darasa la tatu.

Wanafunzi hao wameeleza kuwa, wamekuwa wakipewa msaada na ushauri kutoka kwa wazazi au walezi wao namna ya kutumia njia hizo za uzazi ili wasikatishe masomo pindi watakapopata ujauzito.

“Hapa unapotuona karibu kila mmoja wetu ana mpenzi wake, lakini hatubebi mimba kwasababu tunatumia vipandikizi na wengine sindano za majira ilimradi tuwe salama.” Mwanafunzi wa kidato cha pili.

Mmoja wa wazazi katika Wilaya hiyo, Bi Khadija Mmboga amesema kuwa wazazi hulazimika kuwasaidia watoto kutumia njia hizo ili wamalize masomo yao kwani wasipowasimamia kufanya hivyo wataharibu maisha yao yajayo.

Dkt. Kibamba kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anashauri kuwa wanafunzi wasitumie dawa za aina yoyote kuzuia ujauzito kwakuwa uwezekano wa kuharibu mifumo ya uzazi watakapokuwa wakubwa ni mkubwa, badala yake watumie mipira ya kike na kiume kama itabidi.

Send this to a friend