Viashiria 5 vya Ngozi vinavyoonesha kuwa moyo uko kwenye hatari 

0
57

Kama kiungo chako kikubwa na pekee kinachoonekana nje, ngozi yako ni dirisha la afya yako kwa ujumla. Kuona kitu cha kutiliwa shaka kwenye ngozi yako kunaweza kuwa mojawapo ya dalili za kwanza kwamba kuna kitu kibaya kwenye kiungo chako kingine, ikiwa ni pamoja na moyo wako.

Hivi ni viashiria vitano vya Ngozi yako vitakavyokupa taarifa kuwa moyo wako uko katika hatari.

1. Mabadiliko ya rangi ya ngozi

Mabadiliko ya rangi hasa kwenye vidole vyako au midomo wakati mwili wako una joto, inaweza kuonyesha tatizo la moyo. Kushindwa kwa moyo hutokea wakati misuli ya moyo haisukumi damu vile inavyopaswa. Mtiririko mbaya wa damu unaweza kusababisha ngozi kuonekana bluu (cyanotic).

Rangi ya zambarau kwenye ngozi ambayo hudumu hata katika hali ya joto zaidi inaweza pia kuwa alama hatari. Hii inajulikana kama ‘livedo reticularis’, na kawaida huonekana kwenye mikono au miguu.

 

2. Ukuaji wa rangi ya njano
Wasiliana na daktari ikiwa unaona  matuta ya njano au ya rangi ya machungwa kwenye ngozi yako. Yanaweza kutokea popote kwenye mwili lakini mara nyingi hupatikana kwenye viungo kama magoti na viwiko vyako au hata kwenye kope. Unaweza kuonekana kama upele  kwa mtazamo wa kwanza, lakini kwa kiasi kikubwa ni mkusanyiko wa mafuta chini ya ngozi inayoonyesha kiwango cha juu  cha ‘cholesterol’ katika damu.

3. Kuvimba miguu na vifundo
Kuvimba kwa miguu na vifundo inaweza kuwa dalili nyingine ya ugonjwa wa moyo. Moyo unapodhoofika, hauwezi kusukuma damu kwa ufanisi kupitia mishipa hadi maeneo kama vile miguu na mgongo, na kusababisha mkusanyiko. Hii ina maana kwamba hukusanyika kwenye miguu, na maji hutoka nje ya mishipa ya damu kwenye tishu zinazozunguka.

4.Kujikuna
Mkusanyiko wa maji ambayo husababisha ngozi kuwa nyekundu, kuwasha, na hata kuacha magamba inaweza kusababishwa na utendaji usiofaa wa moyo, kwani damu hushindwa kusafiri vizuri kupitia mishipa.

5. Madoa mekundu
Hujidhihirisha kwenye ngozi kama madoa mekundu-zambarau. Kawaida si laini na hutokea kwenye viganja na nyayo za miguu. Alama hii pia inaweza kuwa hatari na inaweza kuashiria matatizo ya moyo pia.