Ikiwa umewahi kunywa pombe nyingi wakati wa usiku, basi unaelewa nini kinaweza kufuata wakati wa asubuhi. Kupata kichefuchefu, maumivu ya kichwa, kinywa kuwa kikavu, na uchovu ni ishara tosha kwamba una mning’inio ‘hangover’.
Hizi ni njia 4 za kuondoa mning’inio
Maji
Kama tunavyojua, unywaji wa pombe husababisha safari za mara kwa mara za maliwatoni hivyo maji hupungua mwilini na ndio maana unapata mning’inio.
Hakikisha unakunywa maji mengi. Maji ni mojawapo ya tiba bora zaidi ya mning’inio lakini jaribu kutokunywa haraka sana, vinginevyo unaweza kujihisi mgonjwa.
Ndizi
Pombe hupunguza potasiamu. Hivyo kula ndizi au matunda mengine yenye potasiamu nyingi pale unapokuwa na mning’inio, kunaweza kurudisha potasiamu na elektroliti zilizopotea na kukufanya ujisikie vizuri.
Supu
Unapokuwa na mning’inio kunywa supu ili kuondokana nayo. Utafiti wa hivi karibuni wa kisayansi unapendekeza kuwa, supu ya tambi ndiyo bora zaidi, lakini supu yoyote itasaidia pia. Unapokunywa itakutoa jasho ambayo husaidia kuondoa sumu katika damu yako kutokana na pombe.
Kulala
Watu hulala sana baada ya kunywa. Pombe itakufanya ulale haraka. Jaribu kulala siku inayofuata ili kuondoa maumivu ya mwili na kuboresha ubongo wako, kwa kufanya hivyo, itakufanya ujisikie vizuri.