Uganda: Wanandoa wa Marekani wakamatwa kwa kumtesa mtoto wa kuasili

0
41

Mamlaka nchini Uganda imewashitaki wanandoa wawili wenye asili ya Marekani kwa kosa la kumtesa mtoto wao waliomuasili (adopt), mwenye umri wa miaka 10.

Wanandoa hao, wote wenye umri wa miaka 32, walifunguliwa mashitaka siku ya Ijumaa na kuwekwa rumande katika Gereza la Luzira, nje kidogo ya mji mkuu wa Kampala baada ya majirani kutoa taarifa kutokana na mateso ya mara kwa mara aliyokuwa akipewa mtoto huyo anayesoma shule ya watoto wenye mahitaji maalum mjini Kampala.

Mahakama yatupitilia mbali pingamizi la Sabaya na wenzake

Polisi walipovamia nyumba hiyo, walipata ushahidi wa CCTV ukionesha kuwa mtoto huyo alilazimishwa kuchuchumaa katika hali isyokuwa ya kawaida na alipewa chakula cha baridi tu huku akilazwa kwenye jukwaa la mbao bila godoro wala kitanda.

Mvulana huyo alikuwa mmoja wa watoto watatu waliolelewa na wanandoa hao tangu 2020, ambao walifika nchini humo mwaka 2017 kujitolea katika shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake makuu nchini Marekani katika mji wa Jinja kabla ya kuhamia Naguru, kitongoji cha Kampala.

Send this to a friend