Mchungaji Kimaro asamehewa baada ya kuomba msamaha kanisani

0
54

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt. Alex Malasusa ametangaza msamaha kwa Mchungaji wa Ushirika wa Kijitonyama, Dkt. Eliona Kimaro ambaye alipewa likizo ya siku 60.

Msamaha huo umetolewa leo Februari 19, 2023 katika ibada iliyoongozwa na Askofu Malasusa ambapo uamuzi huo umefuata  baada ya Mchungaji Kimaro kupewa fursa ya kuwasalimia waumini na kuomba radhi kwa yote yaliyotokea.

“..Mchungaji Kimaro kama ulivyoomba umesamehewa, endelea kutafakari, endelea kukaa karibu na Mungu wako,” amesema

Akizungumza wakati wa ibada hiyo Mchungaji Kimaro ameomba radhi kwa Askofu Mkuu wa KKT, Dkt. Fredrick Shoo kwa usumbufu wowote uliojitokeza wakati ambao amekuwa likizo.

“Naomba radhi kwa mkuu wa kanisa Askofu, Dk Fredrick Shoo kwa usumbufu wowote ambao ulijitokeza katika mitandao na kwenye vyombo vya habari kwa wakati huu ambao nimekuwa likizo ya faragha,” amesema Dk Kimaro.

 

Send this to a friend