Rais Samia: Wanasiasa tufuate nyayo za Lowassa, tusitukanane

0
50

Rais Samia Suluhu Hassan amewaasa wanasiasa kufuata nyayo za Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa za kuheshimiana na kujenga siasa zenye hoja pasipo kutukanana kwa kuwa huo ndio ukomavu wa kisiasa.

Ameyasema hayo leo katika mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, nyumbani kwake katika Kijiji cha Ngarash Monduli mkoani Arusha ambapo viongozi mbalimnbali wameshiriki mazishi hayo.

“Alipofanya uamuzi wa kuhamia chama kingine, aliendelea kunadi sera zake na kuifafanua dhana ya safari yake ya matumaini bila kumtukana, kumkejeli wala kumzushia mtu yeyote. Hata alivyorudi CCM hakuwahi kuwananga, kuwazodoa na kuwakebehi wala kuwasema vibaya kule alikotoka upinzani,” amesema.

Amesema Hayati Lowassa ameacha funzo kuwa wanasiasa wanaweza kutofautiana mitazamo, misimamo na sera pasipo kulumbana, kutukanana “wala kutikisa misingi ya utaifa na mshikamo wetu na bado tukaelewana” na hivyo taifa likabaki salama.

Naye, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Hayati Lowassa alikuwa kiongozi mwadilifu mwenye maono na mapenzi kwa nchi yake hivyo Watanzania wanapaswa kuyaenzi mazunri yake na kumwombea.

Send this to a friend