Dereva bajaji aliyekimbia polisi Ubungo akamatwa

0
4

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia John Mosha (30), dereva bajaji na mkazi wa Kimara Temboni kwa kosa la kupita katika barabara ya mabasi ya mwendokasi.

Katika taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema wakati wa ukamataji dereva huyo alikaidi kukamatwa na kuamua kuendesha bajaji kwa mwendokasi bila kusimama hadi maeneo ya Ubungo Mawasiliano alipokamatwa, ambapo baadaye madereva bajaji wenzake walifika na kuanza kuwazuia askari polisi kumshikilia dereva huyo.

“Mmoja kati ya madereva hao alichomoa plag ili isichukuliwe na polisi kitendo kilichosababisha cheche na hatimaye moto kuwaka kwenye bajaji hiyo,” imesema taarifa.

Aidha, Jeshi la Polisi limetoa onyo kwa madereva wote wa vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani na kuacha mara moja kupita kwenye barabara za mwendokasi isipokuwa kwa magari yaliyoruhusiwa kisheria.

Send this to a friend