
Watu wengi wanajua kuwa kunywa pombe bila kula chakula ni hatari kwa afya, lakini wachache wanatambua kuwa si salama kuchanganya kifungua kinywa na pombe. Kunywa pombe nyingi asubuhi kunaweza kukusababishia magonjwa, na endapo hutakuwa makini, unaweza kuishia kupata magonjwa makubwa ya ini, figo na utumbo.
Mshauri Mwandamizi wa Upandikizaji wa Ini, Kongosho na Utumbo pamoja na Upasuaji wa HPB katika Hospitali ya Global, Mumbai, Dkt. Hunaid Hatimi, anasema ikiwa mtu anahisi kwamba jambo la kwanza la kufanya kila asubuhi ni kunywa pombe ili kuweza kukabiliana na siku, hiyo ni dalili ya utegemezi wa kisaikolojia kwa pombe.
Hizi ni sababu za kwanini hupaswi kunywa pombe asubuhi;
1. Huathiri utendaji wa kazi na majukumu ya siku
Kunywa pombe mapema kunakufanya ushindwe kuzingatia kazi, shule au majukumu ya familia.
Inaweza kupunguza kasi ya kufikiri na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.
2. Inaashiria utegemezi wa pombe (uraibu)
Mara nyingi watu wanaokunywa asubuhi huonyesha dalili za utegemezi (alcohol dependence), hali ambayo ni hatari kiafya na kijamii.
3. Huongeza hatari ya ajali
Ukinywa asubuhi halafu ukaendesha gari au kutumia mashine, uko kwenye hatari kubwa ya kusababisha ajali kwa sababu akili haitakuwa timamu.
4. Huathiri mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Mwili bado uko katika hali ya kutuliza viungo baada ya usingizi. Kunywa pombe wakati huo kunaweza kuathiri ini, tumbo, na utumbo.
5. Huathiri heshima na mahusiano
Kunywa pombe asubuhi huonekana kama tabia isiyofaa kijamii. Inaweza kuharibu taswira yako mbele ya watu wa karibu na jamii.
6. Huathiri afya ya akili
Inaweza kusababisha hisia za huzuni, kuchanganyikiwa au wasiwasi baadaye, hasa ukinywa mara kwa mara wakati wa asubuhi.