Njia nne za kutengeneza mahusiano mazuri na pesa yako

0
37

Na Kirutu Korosso, Mafia Island, 30.03.2020

Hakuna mtu ambaye hafahamu kwamba mahusiano yetu na pesa ni mahusiano fulani muhimu sana. Tunahangaika kwa njia zote kutafuta pesa ili ifanye maisha yetu na ya wale tuwapendao kuwa mazuri. Tunatumia muda mwingi sana kwenye maisha kuiwaza pesa, ukiwa nayo pia unawaza namna ya kuwa nayo nyingi zaidi na ukiwa huna unawaza zaidi utaipataje.

Tumesoma makala nyingi, video nyingi na kusikiliza podcasts kibao za mambo ya pesa. Ishu ya kwanza lazima kujua ni kwamba huwezi kuwa na mahusiano mazuri na pesa kama huipendi. Yes, you must love money. Huna au unayo, lazima kwanza uipende kama unataka kuhusiana nayo. So mimi hapa nimekusanya kama ishu 4 hivi za kukusaidia mahusiano yako na pesa yawe mazuri. 

Ishu ya kwanza ni commitment. Ili pesa ikupende ukiipangia mipango lazima uitekeleze. I mean, kama kwa mfano umesema mwezi huu nikipata laki zangu tatu, laki moja naweka akiba basi lazima ukipata hiyo laki tatu, uweke akiba hiyo laki moja uliyopanga. Ukianza kuzingua tu kwenye kutotunza ahadi unazoipa pesa yako ujue mahusiano yenu yatavurugika. Umenisoma? 

Ishu ya pili ni kujitengea muda wa wewe na hela yako. Kwenye mahusiano hii ni ile tunaita spending time together na mpenzi. Huu muda unaotenga wa wewe na hela yako ni ule muda unatumia kutafakari matumizi na mipango yako na kuangalia unapoelekea. Kama evaluation time. Hii ni muhimu sababu inakufanya uone kama kuna sehemu ulikosea na vipi ufanye freshi. 

Ishu ya tatu ni kuwa na shukrani. Hizi ni zile moments za kushukuru kwa kufikia lengo fulani la kifedha. Wanasaikolojia wanasema moyo wenye shukrani kwenye mambo ya fedha unapofikia lengo fulani una uwezo wa kuweka malengo zaidi na kuyafikia. Usiwe mtu wa kulalamika miaka nenda miaka rudi. Ukipata shukuru then endelea kukaza kupata zaidi. You feel that?

Ishu ya nne ni kuwa muaminifu kwa pesa yako. Usiishi nje ya uwezo wako maana hiyo ni sawa na kuchepuka na ukichepuka kwenye mahusiano ni tatizo. So kama ilivyo kwenye mahusiano, kuchepuka kwenye ishu ya pesa ni pale unapotumia pesa eidha yote unayopata au zaidi ya unayopata (maana yake unaanza kuwa na madeni). Ukiwa na style hiyo lazima pesa ikukimbie tu maana huna uaminifu nayo. 

Follow me on Twitter @KorossoKirutu

Send this to a friend