Star Media, Multichoice na Azam zapigwa faini kwa kupotosha kuhusu corona

0
15

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeyatoza makampuni ya Azam Digital Broadcasting Limited, Star Media TLD na Multichoice TLD faini ya shilingi milioni tano (5, 000, 000) kila moja kwa kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu virusi vya Corona.

TCRA imefikia uamuzi huo baada ya kubaini ukiukwaji wa Kanuni ya 22(e) ya Kanuni za Miundombinu ya Utangazaji Dijitali na Miundombinu Mingine ya Utangazaji za mwaka 2018, kwa kurusha taarifa ya kituo cha televisheni zenye upotoshaji kuhusu msimamo wa Tanzania juu ya Virusi vya Corona (COVID-19),” imesema taarifa kwa umma iliyochapishwa gazetini.

Vyombo hivyo vimekubali mashtaka na kutakwa kuomba radhi umma mara saba, kwa muda ule ule ukiukaji ulitokea na kulipa faini ya Tshs 5, 000, 000 ndani ya siku 30.

Send this to a friend