Wanamuziki Cheed na Killy wajitoa katika lebo ya Alikiba
Wanamuziki Rasheed maarufu Cheed na mwenzake Ally Omary maarufu Killy wametangaza kujiondoa chini ya lebo ya mwanamuziki Alikiba, Kings Music Records.
Wasanii hao wamesema hawakuwahi kuwa na ugomvi na Alikiba na kuwa hawajaondoka chini ya lebo hiyo kwa ugomvi na kwamba wataendelea kushirikiana na aliyekuwa bosi wao, kwani wamechukua uamuzi huo wakiwa na akili timamu, bila kushawishiwa na mtu yeyote.
“โฆnapenda kuwajulisha fans wangu watu wangu wote waliokuwa wakisupport mziki wangu na wanaoendelea kussuport kazi zangu na hata wasiosupport pia ni kwamba kuanzia leo hii napenda kutamka kuwa mimi sio tena msanii wa @kingsmusicrecords,” wameandika wasanii hao ujumbe uliofanana kupitia kurasa zao za Instagram.
Aidha, mbali na kumshukuru Alikiba kwa kuwasaidia katika kazi zao za kumuziki, wamemtakia kila la kheri katika shughuli zake.
Hapa chini ni jumbe walizoadika wasanii hao kwenye kurasa zao za Instagram: