Utafiti: Waafrika wengi watateseka njaa serikali zikiweka ‘lockdowns’

0
14

Nchi mbalimbali zikiendelea kuchukua hatua mbalimbali kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona, mbili ya tatu ya watu walioohojiwa katika utafiti uliohusisha nchi 20 za Afrika wamesema wataishiwa na chakula na maji endapo watatakiwa kukaa ndani siku 14.

Utafiti huo uliofanywa na Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kupambana na Magonjwa (CDCP) umelenga kuzisaidia serikali za nchi mbalimbali kutambua hatua madhubuti za kuchukua kukabiliana na janga la corona.

Kituo hicho kimetahadhari kuwa endapo mikakati ya kukabiliana na corona haitaendana na hali ya maisha ya watu wa eneo husika, huenda vurugu zikatokea.

Utafiti huo uliofanyika katikati mwa Mwezi umehusisha miji 28 kutoka nchi 20, ambapo umeangazia mtazamo wa watu kuhusu makatazo ambayo tayari yamewekwa na baadhi ya nchi.

Kwa mujibu wa utafiti huo, nyumba zenye kipato kidogo cha fedha, zitakuwa hazina chakula chini ya wiki moja endapo serikali itaamua kufunga maeneo yao (lowackdown).

Miongoni mwa mapendekezo ya utafiti huo ni serikali kuona haja ya kuwasiliana kwa karibu na wananchi na kuwaeleza sababu ya kila hatua ambayo inaichukua kukabiliana na virusi vya corona.

Nchi nyingi za Afrika zimekumbana na changamoto kubwa katika kuamua hatua za kuchukua kudhibiti corona, kwani idadi kubwa ya wananchi wake hutegemea kupata kipato cha siku kwa kutoka kwenda vibaruani.

Send this to a friend