Virusi vya corona huenda visiishe kabisa, WHO imetahadharisha

0
21

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa virusi vya corona huenda visiishe kabisa, huku likitoa tahadhari dhidi ya wanaojaribu kueleza lini virusi hivyo vitapotea.

Mkurugenzi wa kitendo cha dharura cha WHO, Dkt. Mike Ryan amesema hata kama chanjo ya virusi hivyo itapatikana, kuweza kuvimaliza kabisa itahitajika nguvu kubwa sana.

“Ni muhimu hili likafahamika, virusi hivi vinaweza kuwa ugonjwa mwingine tutakaokuwa nao kwenye jamii, na huendi isiishe kabisa. Virusi vya UKIMWI havijawahi kutokomea, lakini tumepata njia ya kuishi navyo,” amesema Dkt. Ryan akizungumza katika mkutano jijini Geneva.

Amesema licha ya kuwepo chanjo zaidi ya 100 zinazoendelea kufanyiwa majaribio duniani kote, haimaanishi kwamba zitaumaliza ugonjwa huo kwani yapo magonjwa mengi yanye chanjo lakini bado yapo katika jamii zetu.

Zaidi ya watu milioni 4.3 wameripotiwa kuambukizwa virusi hivyo duniani kote, waliopona wakiwa ni milioni 1.7, huku takribani 300,000 wakifariki.

Send this to a friend