Taarifa ya wizara afya kuhusu kupungua kwa wagonjwa wa corona Tanzania

0
11

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Mabula Mchembe amesema idadi ya watu waliopata maambukizi ya wagonjwa wenye maambukizi ya virusi vya corona kwenye baadhi ya vituo vya matibabu imepungua na wengi wao wanaendelea vizuri

Akitaja idadi ya wagonjwa katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani amesema katika Hospitali ya Amana kuna wagonjwa 12, Mloganzila wagonjwa 6, Lulanzi mjini Kibaha kuna wagonjwa 24 ambao wengi wao wana hali nzuri.

Amesema kuwa katika hospitali binafsi kuwa wamepata ushirikiano mkubwa na kwamba mbali na kuwepo wagonjwa wa corona, lakini pia wagonjwa hao wanasumbuliwa na maradhi mengine.

Aidha, Mchembe amewasisitiza wahudumu wa afya kuendelea kutoa huduma kwa wagonjwa wote bila ubaguzi.

Send this to a friend