Mambo yanayosababisha gari kutumia mafuta mengi
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetoa bei elekezi za mafuta ambazo zimeanza kutumika leo Desemba 7, 2022. Bei hizo zinaonekana kuwa nafuu kwa wamiliki wa vyombo vya moto kwani imepungua ikilinganishwa na bei ya mwezi uliopita, hasa ikichangiwa na ruzuku ya serikali.
Kwa mujibu wa EWURA kwa mafuta yaliyopokelewa kupitia bandari ya Dar es Salaam, bei ya petroli ni TZS 2,827, dizeli ni TZS 3,247 na Mafuta ya Taa ni TZS 3,252.
Bei ya mafuta kwa mikoa yote kwa Desemba 2022
Mafuta ni kimiminika muhimu sana kwenye gari. Ili gari liweze kufanya shughuli zake zilizokusudiwa ni lazima liwe na mafuta. Uwepo wa mafuta hulifanya gari kutekeleza majukumu yake kama vile kuiwezesha mifumo mbalimbali ya gari kufanya kazi kwa ufasaha na kulifanya gari kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Kwa kawaida kila gari hutumia kiwango fulani cha mafuta kwa kilomita moja, kulingana na ukubwa wa injini na umri wa gari lenyewe. Ikiwa gari linatumia mafuta zaidi ya kiwango ilichotakiwa kutumia kwa umbali fulani, basi yawezekana kuna tatizo linalosababisha kuongezeka kwa kiwango cha mafuta kitumiwacho.
Mambo usiyotakiwa kufanya unapoendesha gari la automatic transmission
Mkurugenzi Mkuu wa Evolution Garage, Evodius Alex anaeleza ni vitu gani ambavyo husababisha gari kutumia mafuta mengi.
Kuchoka kwa Plug
Ni muhimu kubadilisha plugs kwa wakati hasa zikianza kuonyesha hitilafu, mfano gari kutetemeka kwa mbali na hata wakati mwingine zikitumika kwa miezi 6 mpaka mwaka mmoja au zaidi ya kilomita 15000. Plugs huhusika katika uchomaji wa mafuta hivyo uchakavu au kuchoka kwa vifaa hivi huchangia kwa kiasi kikubwa ulaji wa mafuta kwa kiwango kikubwa katika gari.
Matatizo ya umeme katika gari.
Kama gari lina tatizo la umeme, mfano linazimika kila mara, au sensor mbovu au linaonyesha check engine katika dashboard na haujaangalia matatizo haya husababisha gari kula mafuta mengi zaidi. Hii ina maanisha kwamba gari haliko vizuri kaatika mfumo wake wa umeme na hivyo husababisha kutumia mafuta zaidi ukizingatia umeme ni sawa na damu katika mwili wa binadamu. Ni muhimu kuwaona wataalamu wa magari wapime na Diagnosis mashine kujua tatizo lake ili kuepuka ulaji wa mafuta zaidi.
Aidha kama gari lina tatizo la mechanics katika injini, mfano linapandisha joto kila mara ni muhimu kushughulikia tatizo hilo mapema. Ni muhimu pia kujua kiwango cha juu cha joto la gari yako ili utambue kwa haraka joto likizidi kuliko kawaida. Joto likizidi husababisha gari kutumia mafuta mengi zaidi kutokana na kukosa nguvu halisi ya injini. Kuna vitu vingine vya kuangalia kama vile Piston, kiwango cha maji ya Radiator (coolant), ufanyaji kazi wa feni na Thermostat (cooling system).
Kiwango cha RPM anachotumia dereva
RPM ni mzunguko wa injini kwa kipimo cha dakika (Revolution Per Minute). Endapo dereva atakuwa na tabia ya kupenda kukanyaga mafuta zaidi, hii nayo husababisha gari kutumia mafuta mengi hasa magari ya manual. Ni muhimu kuzingatia mafuta unayokanyaga. Matumizi makubwa ya RPM yanaweza kuongeza hadi 3% zaidi ya kawaida. Aidha ni muhimu pia kurekebisha level ya RPM yako hasa unapowasha gari. Magari mengi, RPM zipo katika range ya (0-1) na si zaidi ya hapo pindi tu unapoliwasha. Ukiona mshale wako wa RPM uko juu ya moja na kuendelea wakati gari halitembei, ujue gari linatumia mafuta zaidi ya kawaida.
Matumizi ya Overdrive (OD) kwenye Magari Automatic
Hii nayo husababisha ulaji wa mafuta, ni kweli ukiweka overdrive gari inakuwa nzito na inavuta sana. Unashauriwa kutumia katika safari ndefu, wakati unataka kuovertake au gari inaposinzia kwenye mlima. Kwenye tope au mchanga tumia D2 au Low-L na baada ya hapo rudisha katika Drive ya kawaida-D. katika maeneo ya mjini usitumie OD kwani itaongeza ulaji wa mafuta sana, yaani inatakiwa kuwa ON, dashboard light itakuwa OFF. OD ON inamaanisha kuweka gia za juu haraka na kupunguza kutumia gia kubwa (za chini) katika matumizi ya kawaida na OD OFF ni kupangua gia, inamaanisha kutoka gia ya juu ili uvute kasi na moja kwa moja utaongeza spidi ya injini (RPM) na kasi na pia itakula mafuta zaidi.
Kufahamu Uwezo wa gari yako, ukubwa na umri wa injini
Unatakiwa kuifahamu gari yako kwa kina kuhusu matumizi ya mafuta, ukubwa wa injini, Mileage na vitu vingine. Hii itakusaidia kuepuka matumizi makubwa ya mafuta katika gari lako.
Pia ni muhimu kufahamu umri wa injini yako pamoja na kufanyia engine overhaul au kubadili mnyororo wake kila baada ya kilomita 100,000, ili kuepuka matumizi makubwa ya mafuta. Kwa kawaida injini inapoanza kuchoka kutokana na kutumika kwa muda mrefu huwa ina tabia ya ulaji wa mafuta.
Kufanya matengenezo kwa wakati
Hiki ni kitu muhimu katika kupunguza ulaji wa mafuta wa kiwango cha juu katika gari yako. Unashauriwa kufanyia matengenezo gari lako kwa kubadilisha mafuta na filters kwa wakati. Kuendesha gari zaidi ya kiwango kilichopangwa kulingana na oil unayotumia inaweza kusababisha ulaji wa mafuta. Ni muhimu pia kutumia oil nzuri na sahihi kwa gari yako. Kuna oil za kilomita nyingi kama vile km 5000 na zaidi. na pia ni muhimu kufahamu vilainishi (Lubricants) sahihi vya gari lako.
Ili kufahamu dereva wako anaendesha katika utulivu na ustadi wa namna gani, unashauriwa kupima kiwango cha mwendokasi (Cruise control) cha dereva husika, hii itakusaidia kufahamu hasa matumizi mazuri ya mafuta. Kwa madereva wa magari makubwa ni muhimu kuendesha gari katika wastani wa spidi ya 25% ya spidi ya jumla ya gari (speedometer readings).
Chanzo: Mwananchi