Katibu Mkuu mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amemuomba radhi Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Dkt. John Magufuli.
Kinana amechukua hatua hiyo kufuatia matukio yaliyojitokeza siku za nyuma ikiwemo mazungumzo ya simu baina yake na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho yakimlenga moja kwa moja Rais Magufuli.
"Utaratibu wa adhabu kwenye chama ni wa kawaida, na mimi nimepata adhabu kama wengine na sitakuwa wa mwisho."- Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana pic.twitter.com/TvIiky0KoP
— Swahili Times (@swahilitimes) June 4, 2020