Teknolojia ya kidijitali inavyoleta mapinduzi ya kiuchumi Tanzania
Katika miaka ya karibuni ukuaji wa teknolojia ya kidijitali umezipa nchi nyingi faida mbalimbali za kibunifu ambazo zinazochochea maendeleo ya watu na ukuaji wa uchumi.
Moja ya teknolojia hizo bunifu ni huduma za afya kidijitali (m-health). Katika nchi nyingi huduma hii imekuwa muhimu ikisaidia watu kupata taarifa za afya na hospitali kutunza kumbukumbu kwa ufanisi zaidi.
Tanzania, huduma hizi za afya kwa njia ya simu zimesaidia watu wengi wazima na wagonjwa kupata taarifa za afya, njia za kujikinga na magonjwa na wakati mwingine hata kupata taarifa za namna ya kuendelea na matibabu, kwa wakati, yote kupitia simu ya mkononi.
Siku za karibuni, tumeona hatua nyingine muhimu kwenye maendeleo ya m-health pale Chuo Kikuu cha Afya cha Aga Khan kilipozindua programu ya kompyuta (app) kutambua dalili za korona. Programu kama hizi zinasaidia sana wakati wa changamoto.
Wakatu tunafurahia matunda ya huduma hizi za kibunifu kwenye sekta ya afya kupitia simu, tukumbuke kwamba kampuni za mawasiliano ya simu za mkononi ni nguzo muhimu katika kufanikisha hilo.
Kampuni kama Tigo Tanzania yenyewe ina mpaka huduma ya bima ya afya kupitia simu ya mkononi ambayo huwapa wateja wake uwezo wa kujiunga na bima ya afya, bima ya maisha, na bima nyingine mbalimbali. Bima hizi huwapa wateja na familia za wahanga wa matatizo malipo ya kifedha pali wanapokumbwa na shida.
Huduma nyingine ya Tigo kusajili vizazi na vifo nayo imerahisisha usajili wa watoto wachanga na kupatikana kwa vyeti vya kuzaliwa kirahisi zaidi. Sote tunajua umuhimu wa cheti cha kuzaliwa kwenye maisha yetu kwenye usajili wa mambo mbalimbali hata kupata ajira.
Huku tukiendelea kufurahia matunda ya uchumi wa kidijitali siku hadi siku, ni jambo la kuvutia kuona kwamba kampuni za simu ziko katika mstari wa mbele kufanikisha utoaji huduma katika sekta ya afya kupitia teknolojia.