Mambo 10 yakuepuka unapokwenda first date

0
12

First date mara nyingi huogofya kwa sababu mara nyingi unakuta humjui kiundani yule unayekwenda naye, kama vile anapenda nini au hapendi nini.

Katika kuondoa ugumu huo, hapa ni vitu 10 ambavyo unatakiwa kuzingatia/hutakiwi kufanya ukienda first date;

  1. Usijikute baharia sana. Mfungulie mlango, sema tafadhali na asante, kula ukiwa umefunga mdomo. Kikubwa hapa uwe mwema, usilete ubaharia mwingi maana hujui kama kutakuwa na date ya pili, hivyo tengeneza mazingira ya kufanya iwepo.
  2. Zingatia usafi wako. Muonekano wa mara ya kwanza (first impression) ina umuhimu sana kwani yote yataamuliwa kutokana na ulivyovaa, unavyozungumza, unavyokuwa. Kwa vile hamjuani, kitakachofanya atake kukujua zaidi ni utakavyo behave siku ya kwanza.
  3. Usiongee wewe kama redio ya mbao. Lengo la date ni wote mfahamiane, sio mmoja awe msikilizaji mwingine mtangazaji. Peaneni muda wa kutosha kila mmoja aeleze sehemu ya maisha yao.
  4. Usikimbilie kumuagizia chakula ambacho hajakwambia, au kuzungumza kwa niaba yake kwani utaona kama haujali mawazo yake.
  5. Kuna wale mpo date lakini anaanza kumsengenya mwenzake, mara umekula sana, au unajishaua hupendi kula. Wewe cha kufanya hata kama kala sana, zungumzia ubora wa chakula na sio wingi wa alichokula.
  6. Hakikisha haulewi kama unatumia pombe. Ulevi unaweza kukupelekea ukasema vitu ambavyo hukutarajia, jua kujidhibiti. Lakini pia usiache kinywaji chako kikiwa wazi mezani, kimalize.
  7. Usilogwe ukaanza kuzungumzia uhusiano wako uliopita katika first date, labda kama amekusisitiza sana mzungumze. Ukimzungumzia sana ex wako, utaonekana kama bado hujaweza ku-move on.
  8. Epuka kujadili mambo ambayo yanaweza kupeleka ugomvi wa mgogoro wowote ule, hasa masuala ya imani.
  9. Usijadili masuala ya ndoa na watoto katika date ya kwanza, mtakuwa na muda wa kutosha huko mbeleni, acheni kutishana na idadi ya watoto unayotaka, sijui uanataka kuoa/kuolewa lini, those might be a deal breaker.
  10. Mgogoro siku zote upo kwenye bili ya date, nani anatakiwa kulipa. Wengi husema aliyeitisha date ndiye alipe, lakini tafiti zinaonesha kuwa wengi hutegemea mwanaume ndiye alipe. Acha kuwa Mpwa wanaolilia kuinuana, lipa bili, akisisitiza sana mgawane sawa, lakini siku zote jiandae kulipa.
Send this to a friend