Matumizi ya overdrive (OD) kwenye gari automatic

0
23

Overdrive ni nini?
Overdrive ni gia katika mfumo wa gari ambayo uifanya gari kuwa katika spidi kubwa huku mzunguko wa injini ukiwa mdogo. Kwa lugha rahisi, OD ni gia ya mwisho inayokupa mwendokasi ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.

Over drive ni kama gia ya ziada itakayokupa mizunguko mingi ya driving shaft kwa mizunguko michache ya engine yako. Unapaswa kuitumia ukiwa unatembea na mwendo mkubwa. Faida zake utatumia mafuta kidogo kwani gari inakwenda kasi kwa mizunguko michache ya engine. Mfano katika gari ya kawaida yani 180km/h ili ufikishe speed 120km/h basi RPM inaweza kua 4000 katka barabara tambarare. Ila ukiweka over drive unaweza tembea speed hiyo hiyo kwa RPM 2000 katika barabara tambarare.

Utajuaje kuwa Overdrive ipo On au Off?
Pindi uonapo taa cha overdrive kwenye dashboard ya gari lako inamaanisha kuwa Overdrive ipo OFF (imezimwa) na pindi taa ya overdrive isipoonekana basi overdrive ipo ON (imewashwa). Overdrive imewekwa kama option yakutumia wakati ukiwa unatembelea speed chini ya 60km/h.

Matumizi ya Overdrive ni yapi?
Unaweza kuitumia pia ikiwa unataka kuipita gari nyingine, mathalani, kwenye kilima ambapo nawe gari yako inakuwa imepungua nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4), na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka ukisha maliza tena matumizi yake.

Eneo lingine, ni mara gurudumu la gari lako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa gari pia.

Watu wengine katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa gari, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogoma kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lililopasuka, nikiwa na maana kwamba hapo gari litakuwa linaacha njia na au kupinduka.

Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya kilomita 70 kwa saa, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo.

Taa ya Overdrive ikiwa hakionekani kwenye dashboard yako maana yake Overdrive ipo Automatic au On na hivyo ndivyo inavopendekezwa na wataalam gari iwe automatic pindi upo mjini na unatembelea speed tofauti (sometimes less or more than 60). Kwa vile overdrive inatumia gear kubwa na spidi chini ya 60km, unaweza kutumia wakati unashuka milima mikubwa.
.

Send this to a friend