Mwanamuziki Rajab Abdul, maarufu Harmonize ameweka wazi mpango wake wa kugombea ubunge katika Jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara, miezi kadhaa baada ya Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli kupendekeza afanye hivyo.
Akizungumza na TBC1, mwanamuziki huyo anayetamba na nyimbo kadhaa ikiwamo Bed Room, amesema kuwa alijisikia furaha sana kuambia hivyo na Rais Magufuli, hadi machozi yalimtoka kwa sababu sio kitu cha kawaida kiongozi wa nchi kumpendekeza raia kugombea jimbo fulani.
“Kama mkuu wa nchi anakuamini, anakuona kabisa you can do this [unaweza kufanya hili], mimi ni nani?” amesesema Harmonize alipoulizwa kama ana ndoto za kugombe ubunge.
Licha ya kuweka wazi kuhusu mpango huo, amesema mambo mengine yanabaki kuwa chini ya kapeti, hivyo hakusema kama atagombea katika uchaguzi wa mwaka 2020 ama la.
Oktoba 2019 baada ya kutumbuiza katika mkutano wa hadhara mkoani Lindi, Rais Magufuli alisema kuwa anatamani kumuona Harmonize akigombea ubunge Tandahimba.
Jimbo la Tandahimba kwa sasa linaongozwa na Mbunge Katani Ahmadi Katani wa Chama cha Wananchi (CUF).
Endapo akagombea na kushinda, ataingia kwenye orodha ya wasanii ambao ni/ wamewahi kuwa wabunge nchini ambao ni pamoja na Joseph Haule (Profesa Jay), Joseph Mbilinyi (Sugu).