Picha: Rais Magufuli akagua ujenzi wa barabara za juu Ubungo

0
37

Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli amekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Barabara za Morogoro, Nelson Mandela na Sam Nujoma na kuelezea kufurahishwa kwake na kazi nzuri inayoendelea.

Rais Magufuli amefanya ukaguzi huo na kuzungumza na amewasalimu wananchi wakiwemo viongozi na wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa waliokuwa wamekusanyika wakati akitokea Makao Makuu, Dodoma.

Rais amewapongeza wananchi wa Ubungo kwa kupata mradi huo na ameeleza kuwa Serikali inatumia zaidi ya TZS 240 bilioni kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara za juu eneo la Ubungo na pia inajenga barabara ya njia nane (Kimara – Kibaha) kwa kuwa imedhamiria kuibadilisha Tanzania. Amewataka Watanzania wote kuunga mkono juhudi hizo.

Baada ya kuwasalimu wananchi hao, Rais Magufuli ameendesha harambee ya kuchangia ununuzi wa pikipiki ya miguu mitatu kwa ajili Nyangoma James ambaye ni mwenye ulemavu, na amefanikiwa kukusanya TZS 8,750,000/- zikiwemo TZS 5,000,000/- alizotoa yeye mwenyewe.

Send this to a friend