Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na wenzake saba wamebadilishiwa shtaka linalowakabili mara baada ya kukamatwa na polisi mkoani Lindi.
Taarifa iliyotolewa na chama hicho inaeleza kuwa awali wanachama hao walikuwa wakituhumiwa kufanya maandamano bila kibali cha polisi, lakini baadae shtaka lilibadilishwa na kuwa kutishia uvunjifu wa amani.
Hata hivyo wanachama hao nane wa ACT Wazalendo wameachiwa kwa dhamana ya wadhamini wawili kila mmoja.
Aidha, washtakiwa hao wametakiwa kuripoti polisi mkoani Lindi Julai 1, 2020.