CHADEMA yaomba polisi kumpatia Lissu ulinzi akirejea

0
23

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kimeliomba Jeshi la Polisi kumpatia Tundu Lissu ulinzi atakaporejea nchini kwa sababu usalama wake bado upo mashakani.

Lissu amesema hayo wakati akizungumza na Watanzania kwa njia ya mtandao ambapo amesema katika miezi sita iliyopita Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aliandika barua mbili kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania kuomba apatiwe ulinzi atakaporudi.

Lissu amesema hadi sasa wanasubiri majibu ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao ndio wenye jukumu la kuhakikisha kuwa yuko salama atakaporejea nchini humo.

Mwanasiasa huyo ambaye anatarajia kurejea nchini kugombe Urais kupitia CHADEMA amesema hawezi kuwa na jeshi binafsi la kumlinda na kwamba wanapopaswa kuhakikisha ulinzi wake ni viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Lissu amesema kuwa watu waliojaribu kumuua Septemba 7, 2020 bado wapo, lakini licha ya hatari hiyo atarejea nchini kwa sababu ndipo nyumbani kwake.

”Kwa hiyo ninarudi nchini kwangu katika mazingira ambayo hatari dhidi yangu haijaondoka bado. Lakini ninarudi tu, ni nyumbani kwetu, inabidi nirudi,” amesema Lissu.

Send this to a friend