Mpishi Kenya avunja rekodi ya dunia

0
14

Mtaalamu wa Mapishi, Maliha Mohammed kutoka Mombasa nchini Kenya amevunja rekodi ya dunia (Guinness World Record) kwa kutumia mrefu zaidi akipika.

Maliha alivunja rekodi hiyo jana Jumapili Agosti 18 baada ya kutimiza saa 75 (sawa na siku tatu na saa 3) akipika bila kupumzika akiwa Kenya Bay Beach Resort.

Awali rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na raia wa Marekani, Rickey Lumpkin kutoka Los Angeles ambaye mwaka 2018 aliweka rekodi kwa kutumia saa 68, dakika 30 na sekunda 01 akipika bila kupumzika.

Maliha mwenye miaka 36 aliandaa aina 400 za viungo mbalimbali vya kitaifa na kimataifa kwa ajili ya shindano hilo.

Chakula alichokiandaa kitatolewa katika vituo vya kulea watoto yatima ikiwa ni njia yake ya kukuza uelewa na kuwasaidia waoishi kwenye mazingira magumu mjiini Mombasa.

Katika jaribio lake la kwanza mwezi Mei mwaka huu, mama huyo wa watoto wawili alitumia saa 36 kupika.

Katika jaribio la pili mwezi Julai mwaka huu, alipika jumla ya vyakula 200 kwa muda wa saa 54, kabla ya kwenda kwenye shindano hilo ambalo alisimamiwa na maofisa kutoka Guinness World Record.

Send this to a friend