Wafungwa miaka 30 kwa kujaribu kumuua Rais mpya wa Burundi
Mahakama nchini Burundi imewahukumu wanaume wawili na mwanamke mmoja kifungo cha miaka 30 jela kwa kutaka kumuua Rais wa nchi hiyo, Evariste Ndayishimiye kwa kuupiga mawe msafara wake.
Mwendesha mashtaka aliiomba mahakama katika Jimbo la Kayanza kuwafunga watu hao miaka saba jela kwa kuhatarisha usalama wa Rais, lakini mahakama iliamua kuwatia hatiani kwa kutaka kumuua kiongozi huyo.
Watatu hao wlikuwa wakituhumiwa kuupiga mawe msafara huo kutokea kwenye eneo lao la kazi wakati kiongozi huyo alipolitembelea, mashtaka ambayo wameyakanusha.
Rais Ndayishimiye alitarajiwa kuingia madarakani Agosti 20 mwaka huu, lakini aliapishwa Juni mwaka huu kufuatia kifo cha aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo, Rais. Pierre Nkurunziza.