AMRI: Wamiliki wa ‘drones’ watakiwa kuzisajili, mwisho Agosti 28, 2020

0
26

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imewataka wamiliki wa ndege zisizo na rubani (drones) kuhakikisha zimesajiliwa ifikapo Agosti 28, 2020.

Taarifa ya TCAA imesema agizo hilo linahusisha ndege zilizopewa kibali awali na ambazo hazijasajiliwa, hatua ambayo ni utekelezaji wa kanuni za kiusalama za kudhibiti matumizi ya ndege zisizo na rubani za mwaka 2018.

TCAA imesema kuwa yeyote atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria ambapo tayari kikosi kazi kati ya TCAA na Polisi kimeundwa kwa ajili ya kusimamia matumizi ya ndege hizo.

Wamiliki wameelekezwa kusajili ndege hizo katika ofisi za TCAA zilizopo maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na Makao Makuu ya TCAA, Dar es Salaam na katika ofisi za kanda.

Pamoja na matakwa mengi, kanuni hizo zinaelekeza kuwa mtu au kampuni kuomba kibali kutoka TCAA kabla ya kuingiza na kusajili ndege hizo. Aidha, wamiliki wanatakiwa kuomba kibali TCAA, kutoa taarifa polisi na serikali za mitaa wakati wa matumizi.

Send this to a friend