Maafisa wa CHADEMA wakamatwa kwa kuchoma moto ofisi za chama hicho Arusha

0
12

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watumishi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanaotuhumiwa kuchoma moto ofisi za chama hicho mkoani humo.

Agosti 14 mwaka huu saa 9:30 usiku raia hao wanadaiwa kuwa walichoma moto ofisi za CHADEMA katika Kata ya Kimandolu, Arusha na kusababisha uharibifu wa mali zenye thamani ya TZS 5.7 milioni.

Taarifa ya polisi imewataja waliokamatwa kuwa ni mlinzi wa ofisi hiyo, Deogratius Malya, dereva wa CHADEMA ambaye ji mkazi wa Dar es Salaam, Leonard Ntukula na Afisa Uhamasishaji wa CHADEMA Makao Makuu, Prosper Makonya.

Baada ya kukamilisha upelelezi, polisi wamepeleka jalada hilo kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa aji ya kulisoma na kulitolea uamuzi au maelezo ya kisheria ikiwa ni pamoja na kuandaa mashtaka.

Aidha, watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikisjwa mahakamani pindi taratibu za kisheria zitakapokamilika.

Send this to a friend