Kombe la Mataifa ya Afrika lapotea nchini Misri
Chama cha Mpira wa Miguu nchini Misri kinaendelea na uchunguzi kubaini lilipo kombe halisi (oroginal) la Mataifa ya ya Afrika ambapo limeripotiwa kupotea pamoja na makombe mengine katika mazingira ya kutatanisha.
Kutokuwepo kwa kombe hilo kulijulikana wakati shughuli za ukarabati wa makumbusho madogo zikiendelea kwenye makao makuu ya chama hicho jijini Cairo.
Taifa hilo limetwaa kombe hilo mara tatu, mwaka 2006, 2008 na 2010 ambapo baada ta mafanikio hayo lilipewa kombe hilo liwe lao.
Mwaka 2013 mashabiki walivamia jengo hilo na kuharibu baadhi ya vitu lakini haijafahimika kama ndipo kipindi ambacho kombe hilo pamoja na mengine yalitoweka.
Chama hicho kimesema baada ya uvamizi huo kilipelekea makombe yote stoo, na kuwa karibuni maafisa wa soka walianza kuyakusanya tena ili kuwekwa makumbusho pindi ukarabati utakapokamilika, ndipo walipobaini baadhi ya makombe hayapo.
Kanuni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zinaeleza kuwa timu itakayoshinda kombe hilo mara tatu, itakabidhiwa na kulimiliki kombe husika.