Wanafunzi 10 wafariki kwa moto Kagera

0
33

Wanafunzi 10 wamefariki dunia na wengine sita wamejeruhiwa baada ya moto kuteketeza bweni la wavulana wa Shule ya Msingi Islamic Byamungu iliyopo Kyerwa mkoani Kagera.

Taarifa kutoka mkoani humo zinaeleza kuwa moto huo umeanza usiku wa kuamkia leo na wanafunzi hao walifariki hapo hapo na majeruhi hao wamepelekwa katika Hospitali ya Nyakahanga.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na kwamba hadi asubuhi leo shughuli kubwa ilikuwa ni kuwapatia huduma ya kwanza wanafunzi wengine na kuendelea kuzima moto, kwani bado kulikuwa na viashiria vya moto.

Bweni hilo pamoja na mali nyingine za wanafunzi zimeteketea kwa moto.

Send this to a friend