Botswana kuanza kutumia Kiswahili shuleni

0
27

Serikali ya Botswana inakusidia kuanza kutumia lugha ya kiswahili shuleni, Waziri wa Elimu ya Msingi, Fidelis Molao amesema.

Akizungumza akiwa mjini Francistown Molao amesema kuwa lugha hiyo itaanza kutumika katika kipindi cha usoni.

Endapo lugha hiyo itaanza kutumika itakuwa lugha ya kwanza ya Kifrika kutoka nje ya mipaka ya nchi hiyo inayoongoza kwa uzalishaji wa almasi.

Kiswahili ni lugha ya Kibantu inayozungumzwa zaidi katika Ukanda wa Maziwa Makuu na sehemu nyingine za Mashariki na Kusini mwa Afrika ikiwa ni pamoja na Burundi, Rwanda, DC Congo, na Malawi.

Kuendelea kukua kwa matumizi ya lugha hiyo kunatajwa kuwa kutakuza biashara na ushirikiano ndani ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ambayo wanachama wake wengi wanatumia lugha hiyo.

Send this to a friend