Wanafunzi kutoka Afrika kuzuiwa kusoma shahada Marekani

0
11

Serikali ya Rais Donald Trump inakusudia kuzuia wananfunzi kutoka katika baadhi ya nchi za Afrika na Asia kusoma shahada nchini Marekani kwa kupunguza muda wanaoruhusiwa kukaa nchini humo.

Hatua hiyo inatokana na pendekezo la Idara ya Mambo ya Ndani ya Marekani ambalo linaelekeza kuwa wanafunzi kutoka katika nchi mbalimbali watapewa kibali cha kukaa nchini humo kwa muda usiozidi miaka miwili.

Hatua hiyo itawaathiri wananfunzi kutoka nchi zitakazowekewa zuio hilo kwani masomo ya shahada nchini humo huchukua zaidi ya miaka miwili kukamilika.

Miongoni mwa nchi nyingi zitakazoathiriwa na uamuzi huo ni kutoka Afrika na nchi zenye migogoro barani Asia.

Wanafunzi watakaoathirika na uamuzi huo ni kutoka Kenya, Rwanda, Uganda, Tanzania, Burundi, Sudan Kusini, Somalia, na Ethiopia.

Mbali na Afrika Mashariki, nchi nyingine za Afrika ni Benin, Burkina Faso, Burundi, Cameroon, Jamhuri ya Africa ya Kati, Chad, DR Congo, Jamhuri ya Congo, Côte d’Ivoire, Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea-Bissau, Liberia, Libya, Malawi, Mali, Mauritania, Niger, Nigeria, Papua New Guinea, Senegal, Sierra Leone, Sudan, Togo, na Zambia.

Barani Asia nchi zilioathiriwa ni Korea Kaskazini, Afghanistan, Bhutan, Guyana, Haiti, Iran, Iraq, Kosovo, Kyrgyzstan, Moldova, Mongolia, Nepal, Papua New Guinea, Ufilipino, Samoa, Syria, Tajikistan, Tonga, Turkmenistan, Tuvalu, Uzbekistan, Vietnam, na Yemen.

Idara hiyo imesema uamuzi huo unalenga kuzuia wanafunzi kuzidisha muda wa kukaa nchini humo.

Taarifa kutoka nchini humo zinazeleza kuwa kwa mwaka 2019 watu 32,023 walidaiwa kuzidisha muda wa kukaa nchini humo.

Send this to a friend