Kusudio la Tigo na Zantel kuungana litaboresha sekta ya mawasiliano ya simu nchini

0
14

Kampuni za mawasiliano ya simu nchini Tanzania zimekuwa na mchango mkubwa sana katika kuhakikisha kuwa nchini inasonga mbele kimaendeleo.

Kampuni hizo zimekwenda mbali zaidi na kutoa huduma zenye ubunifu mkubwa kama vile huduma za kifedha kwenye simu. Kwa siku za hivi karibuni huduma hiyo imesaidia biashara ndogo na za kati (SMEs) kwa kuzisaidia kupata huduma za kifedha na usimamizi wa fedha zao.

Hata hivyo, hofu imezuka kuwa soko la sekta ya mawasiliani nchini limekuwa na washiriki wengi, na hivyo kupelekea kuwepo ushindani usio na tija. Soko la mawasiliano nchini Tanzania ndilo lenye washiriki wengi zaidi Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Katika sekta nyingine, idadi kuwa ya washindani kwa nyakati nyingine huwa na manufaa kwa watoa huduma pamoja na wateja wao. Lakini, hali haiku hivyo katika sekta ya mawasiliano ya simu.

Tafiti zimeonesha kuwa kupunguza idadi ya kampuni zinotoa huduma ya mawasiliano ya simu, husaidia kampuni chache zitakazosalia kuwekeza zaidi katika kukuza teknolojia yake na huduma kwa wateja, hatua ambayo huboresha utoaji huduma.

Katika taarifa za hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa Tigo na yule wa Zantel walieleza kusudio lao la kuunganisha kampuni hizo, kwa lengo la kuimarisha kampuni zote mbili.

Kwa kuziunganisha Tigo na Zantel, wateja wa sasa wa Zantel wataweza kutumia huduma bora ambazo tayari wateja wa Tigo wanazifurahia kama vile Tigo Pesa. Hii ina maana kuwa wafanyabiashara wengi wadogo na wa kati wataweza kutumia huduma za fedha kwenye simu zinazotolewa na Tigo, hatua itakayosaidia kukuza biashara hizo.

Tupokee kwa mikono miwili uamuzi wa kuziunganisha kampuni hizi mbili, na kuzisaidia katika mkakati wake wa kukuza uchumi wa Tanzania.

Send this to a friend