Waziri wa Afya wa Kenya ameonya kuwa huenda nchi hiyo ikaingia katika awamu ya pili ya maambukizi ya virusi vya corona kutokana na ongezeko la kasi ya maambukizi mapya.
Mutahi Kagwe amesema maambukizi mapya yameanza baada ya Rais Uhuru Kenyatta kulegeza masharti ya kukabiliana na #COVID19.
Kasi ya maambukizi imeongezeka kufikia 12% kutoka 4% mwezi uliopita. Kagwe amesema pia kumekuwa na ongezeko la watu kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU).
Amelaumu watu kutokaa kwa umbali unaotakiwa na kutovaa barakoa hasa kwenye baa na mikutano ya kisiasa kama chanzo cha maambukizi mapya.
Akitoa mfano, ameurushia lawama wimbo wa Jerusalema kuwa ni chanzo cha maambukizi ya #COVID19 nchini humo kwani watu wanacheza wimbo huo kwenye baa na kumbi za burudani bila tahadhari ikiwemo kuvaa barakoa na kukaa kwa umbali.
Nchi hiyo imeripoti visa zaidi ya 44,800 ambao kati ya hivyo, watu 832 wamwfariki dunia.